Menejmenti ya
Hifadhi za Taifa -TANAPA- imeshauriwa
kuanzisha utaratibu wa kutoa zawadi kwa watalii wa ndani,watakaofanya vizuri
kwa vigezo vitakavyowekwa watakaotembelea hifadhi zake ,ukiwemo Mlima
Kilimanjaro.
Rai hiyo
imetolewa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi,Prof esa FAUSTIN BEE katika kilele cha tatu cha Mlima Kilimanjaro
cha Shira,katika siku ya mwisho ya kampeni ya kuwahamasisha Watanzania kupanda
mlima huo.
Prof esa BEE
amesema, utaratibu huo utasaidia kuwahamasisha Watanzania , hasa vijana kutembelea hifadhi hizo,kutokana na
idadi ndogo,ya asilimia tano ya watalii
wote waliotembelea hifadhi za taifa ambao ni Watanzania kwa miaka kumi
iliyopita.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi Marangu ,Bwana INOCENT SILAYO amesema, ataishauri Menejment
i ya
Benki ya CRDB kuandaa programu ya
kila mwaka ya watumishi ya benki hiyo kupanda mlima huo kuwahamasisha
Watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea hi fadhi hizo na kujenga afya zao.
Afisa Masoko wa KINAPA,Bwana ANTIPUS MGUNGUS amesema, hifadhi hiyo kwa
sasa inaandaa mpango wa kwenda kwenye taasisi mbali mbali vikiwemo vyuo vikuu
vilivyopo Mkoani Kilimanjaro na mikoa mingine,kuwahamasisha Watanzania kupand a mlima huo badala ya kuwaachia
wageni.


0 comments:
Post a Comment