Wananchi wa Kijiji cha Longuo A Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro wanaka biliwa na tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi kutokana na kamati iliyoundwa kushughulikia kero ya maji katika kijiji hicho kujimilikishaa mradi wa maji ulioibuliwa na wananchi kwa kuwatoza kiasi cha Shilingi Milioni 3 ili kuunganishiwa huduma ya hiyo .
Wakizungumza katika mkutano wa kijiji wananchi hao wa me sema tatizo la maji katika
kjiji hicho limedumu kwa muda mrefu na kusababisha adha kubwa kwa wananchi wa
kijiji hicho kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji safi .
Kufuatia tatizo hilo wananchi hao wameiomba Serikali kutatua kero ya maji katika kijiji hicho kutokana na viongozi mbalimbali kufikia katika kijiji hicho na kuahidi
kutatua tatizo la maji bila mafanikio .
Kwa upande wake mweneykiti wa kijiiji cha Longuo A,Bwana PAUL KISIMA amekiri kuwapo kwa tatizo hilo
na kusema kuwa wananchi hao walitumia gharama kubwa kuibua mradi huo pamoja na
kuchangia nguvu kazi na fedha .
Mhandisi wa maji Wilaya ya Moshi BROMEN LYIMO
amesema Serikali ya wilaya inatambua
mgogoro huo na kwamba malalamiko ya wananchi hao ni ya msingi kutokana na
kutozwa fedha nyingi za kuunganishiwa
huduma ya maji ambayo hayatoshelezi .

0 comments:
Post a Comment