Wahamiaji haramu 23 kutoka nchini Burundi
wamekamatwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Geita wakiwa safarini kuelekea katika
mikoa ya Shinyanga na Tabora kujitafutia hifadhi kutokana na hali tete ya
usalama inayoendelea nchini mwao.
Afisa uhamiaji mkoa wa Geita Charles
washima amesema kati ya wahamiaji hao 23 mmoja ameshashitakiwa mahakamani na
kuhukumiwa kwenda jela miezi tisa kutokana na kupatikana na hatia ya kuingia
nchini kinyume cha sheria, aidha kati ya wahamiaji haramu waliokamatwa wengi
wao ni watoto wadogo chini ya umri wa miaka kumi na nane ambapo idara
hiyo inaandaa utaratibu wa kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo
wake.
Baadhi ya wahamiaji haramu hao kutoka
burundi wamesema wamelazimika kukimbia nchini mwao kutokana maisha magumu na
hali ya vurugu zinazoendelea kwa wananchi kupinga rais wa nchi hiyo Pierre
Nkurunzinza kuingia katika awamu ya tatu ya kuwania kugombea kiti cha urais.
Aidha mkuu wa kitengo cha udhibiti wa
mipaka mkoa wa Geita Vitalis Komanya amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa
ulinzi wa mipaka ya nchi kutokana na kuwa wahamiaji wengi wao huingia nchini
kwa kupitia njia za panya na kuhifadhiwa na wananchi hivyo kuhatarisha usalama.


0 comments:
Post a Comment