Hatua kali zimechukuliwa. Hatua hizo ni pamoja na
kupokonya na kuharibu meli zitakazokua zikitumia katika safari hizo.
Lengo muhimu la opereshini Navfor Med ni kukomesha
biashara ya watu. Operesheni hiyo inalenga pwani za Libya, ambazo zinachukuliwa
kama maeneo muhimu ya biashara ya wahamiaji. Shabaha ni kutoa ulinzi kwa Bahari
ya Mediterranean na kuwaokoa wahamiaji waliokua wakikabilia na ajali mbalimbali
katika bahari. Lakini kwanza kupata taarifa kwa kutumia Satelaiti, rada na
uchunguzi wa angani ili kutafuta njia inayotumiawa na wahamiaji.
Mawaziri wa Mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya
wamekubaliana kuunda jeshi la pamoja la majini ili kuzuia wahamiaji haramu
wanaosafirishwa barani Ulaya wakitokea nchini Libya kupitia Bahari ya
Mediterranean.
Mkuu wa Mambo ya nje wa Umoja huo Federica Mogherini
amesema kuwa jeshi hilo litazinduliwa rasmi mwezi ujao na makao yake makuu
yatakuwa ni mjini Rome nchini Italia.
Maelfu ya wahamiaji haramu wengi kutoka barani
afrika wamepoteza maisha baada ya boti walizosafiria kuzama wakiwa baharini.

0 comments:
Post a Comment