Maandamano hayo yaliyoitishwa na serikali
yamefanyika siku moja baada ya maandamano mengine makubwa yaliyoitishwa na upinzani
ukiomba kujiuzulu kwa Nikola Gruevski. Wafuasi wa upinzani wameendelea kupiga
kambi Jumatatu jioni wiki hii mbele ya makao makuu ya serikali.
Kiongozi mkuu wa upinzani Zoran Zaev, amefichua
rekodi ya mazungumzo ambayo ilionekana kuonyesha udhibiti wa karibu wa viongozi
juu ya waandishi wa habari, mahakimu, na juu ya taratibu za uchaguzi.Hatua hizo
za uchunguzi zinasadikiwa kulenga watu wapatao 20,000. Wapinzani lakini pia
washirika wa utawala. Waziri mkuu hakukana usahihi wa yaliyomo katika rekodi hiyo,
lakini amekanusha kuwa na udhibiti juuu ya watu hao.
Kiongozi huyo wa upinzani, tangu wakati huo
alifuatiliwa kwa kosa la “ unyanyasaji dhidi ya serikali “. Lakini wengi
miongoni mwa raia wanampinga waziri mkuu wakitaka ajiuzulu. Zaidi ya mahema
thelathini yamejengwa tangu Jumapili mwishoni mwa juma lililopita mbele ya
makao makuu ya serikali.
Hata hivyo waziri mkuu Nikola Gruevski haonekani
hata kidogo kuwa ataachia ngazi. Nikola Gruevski alirejea madarakani kwa muhula
mmoja wa miaka minne wakati wa uchaguzi wa wabunge uliyofanyika mwezi Aprili
2014. huku akisema kuwa hana nia ya kujiuzulu.
Wakati huo huo mazungumzo yameanzishwa chini ya
mwumvuli wa Umoja wa Ulaya na Marekani ili kutafutia suluhu mzozo huo wa
kisiasa unaoendelea nchini Makedonia.

0 comments:
Post a Comment