Kompyuta hizo ambazo zinaambatana na huduma za bure za
Internet isiyo na kikomo zimetolewa na kampuni ya Huawei Tanzania kwa
ushirikiano na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa lengo la kuijengea uwezo
Hospitali ya Sekou Toure katika utunzaji wa kumbukumbu za afya, ambapo serikali
kupitia kwa mkuu wa wilaya ya nyamagana Baraka Konisaga imetoa pongezi za dhati
kwa makampuni hayo kutokana na michango yao mbalimbali kwa jamii.
Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo, meneja mkuu
wa Tigo Diego Gutierrez amesema kwamba msaada uliotolewa kwa hospitali hiyo ya
rufaa ni katika kutekeleza mkakati wa kampuni ya tigo wa kuyabadilisha maisha
ya watanzania ili kuwa ya kidijitali katika maeneo yote, sekta ya afya ikiwa ni
mojawapo, huku afisa mtendaji mkuu wa Huawei Zhang Yongquan akisema kwamba
msaada huo unaonyesha jinsi ambavyo kampuni yake imejitolea kusaidia sekta ya
afya ili iendane na mabadiliko ya kiteknolojia.
Mapema mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa
wa mwanza Sekou Toure Dk. Onesmo Rwakyendela pamoja na mwenyekiti wa bodi ya
Hospitali hiyo Christopher Mwita Gachuma wameshauri Kompyuta hizo zitumike kwa
malengo yaliyokusudiwa ili ziweze kudumu kwa muda mrefu, kwani matumizi mazuri
ya kompyuta hizo yatawahamasisha wadau wengine wa maendeleo kuendelea kuwekeza
misaada yao ya hali na mali katika hospitali hiyo yenye uwezo wa kulaza
wagonjwa 375 kwa wakati mmoja.




0 comments:
Post a Comment