Riyama alisema katika filamu mbalimbali alizocheza amekuwa akitumia maneno ya kashfa, kejeli ambayo yameonyesha kuvutia waongozaji wengi wa filamu nchini kumtumia katika filamu zao.
“Nina kila sababu ya kujivunia maneno machafu ya uswahilini kwani hayo ndiyo yananifanya nipate mialiko mingi ya kuigiza kama nilivyoshirikishwa kwenye filamu mbalimbali na sasa naheshimika kwa maneno hayo ingawa wapo baadhi wanafikiri ndiyo maisha yangu halisi wakati naigiza,” alijieleza Riyama ambaye kwa sasa anatamba katika filamu ya Uwoga.
0 comments:
Post a Comment