Suala la hedhi kwa wasichana
limesalia jambo la siri katika jamii barani Afrika ikiwemo nchini Tanzania
ambapo wasichana wengi wanakabiliwa na changamoto nyingi wakati wa siku zao,
hiyo ni kauli ya John Mfungo ambaye ni mtaalam wa maji, afya na usafi wa
mazingira WASH katika Shirika la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania
alipohojiwa na Idhaa hii.
Amesema kwa mantiki hiyo
UNICEF imechukua hatua mbali mbali ikiwemo kutoa muongozo wa ujenzi wa vyoo ,
kuelimisha walimu na wasichana wenyewe ili kukabialiana na changamamoto
zilizopo.
Bwana Mfungo amesema kwamba
ushiriki wa serikali na wadau ni muhimu katika kuhakikisha kwamba mazingira
bora kwaa wasichana wakati wa hedhi yanafikiwa ili waweze kushiriki kikamilifu
kwenye masomo yao..
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment