Amesema hayo wakati huu ambapo Umoja wa
Mataifa unasema walinda amani wake wanakabiliwa na vitisho zaidi kwa kuwa
wanalinda amani pasipo amani na wengi wakiuawa.
Mathalani tangu kuanza kwa ulinzi wa amani
mwaka 1948 hadi sasa walinda amani 3358 wameuawa na idadi imekuwa ikiongezeka
mwaka hadi mwaka.
Moja ya ujumbe wa wa ulinzi wa amani ambao ni
mkubwa zaidi kuliko zote 17 duniani kote ni ile iliyoko Jamhuri ya kidemokrasia
ya Congo, MONUSCO ambayo kamanda wake mkuu Jenerali Carlos Alberto dos Santos
Cruz anasema nchi ni kubwa na changamoto ni nyingi kwa hiyo..
"Tunahitaji kutumia mbinu mbali
mbali na mikakati mbali mbali mbali kwenye maeneo tofauti hapa nchini. Pia
tunahitaji kutumia mbinu zote ambazo Umoja wa Mataifa unatupatia kutekeleza
majukumu yetu. Na pia nadhani hapa DR Congo Umoja wa Mataifa una fursa ya
kutumia mambo mengi kujifunza.
MONUSCO ina jumla ya watendaji 20, 878 ambapo
kati yao zaidi ya Elfu 19 ni askari.
0 comments:
Post a Comment