Mkutano huo unamulika jinsi ubia unavyoweza
kuimarisha mifumo ya afya, na kujenga uthabiti dhidi ya majanga ya magonjwa ya
kuambukiza.
Kikao kimemulika pia suala la ubia na mchango
wake katika kutimiza ajenda ya maendeleo baada mwaka 2015.
Akihutubia kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson, amesisitiza umuhimu wa ubia na njia mpya za
kukabiliana na matatizo yaliyopo duniani sasa
"Kutoka kwa mlipuko wa Ebola,
hadi kuenea kwa misimamo mikali katili na ugaidi hadi hatari ya mabadiliko ya
tabianchi hadi msururu usiokwisha wa migogoro, ni dhahiri kuwa hakuna taifa
moja au shirika linaloweza kuyatatua matatizo haya peke yake. Naamini kuwa njia
mpya ya kutatua matatizo unahitajika katika dunia ya leo. Ni lazima tuwe na
ubia kwa ngazi zote: kitaifa, kikanda na kimataifa."
Wengine waliohutubia ni Rais wa Baraza la
ECOSOC, Martin Sajdik, na rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton.
0 comments:
Post a Comment