Mratibu
mkazi wa umoja wa mataifa nchini ALVARO RODRIGUES amesema, kutokana na idadi
kubwa ya wakimbizi katika kambi ya nyarugusu, ambayo sasa ina wakimbizi karibu
laki moja kufuatia wakimbizi karibu elfu hamsini toka burundi kupelekwa katika
kambi hiyo, hali ya utoaji wa huduma za kijamii imekuwa ngumu na kwamba hatua
ya serikali kutoa eneo la kujenga kambi mpya litasaidia kuepusha madhara katika
kambi hiyo ambayo sasa ina wakimbizi toka burundi na kongo DRC.
mkuu
wa kambi ya wakimbizi nyarugusu SOSPETER BOYO amesema kutokana na ujio huo,
wamelazimika kufunga shule, na kutumia majengo ya shule na viwanja vya michezo
kuwahifadhi jambo ambalo limeanza kuleta mgongano kati ya wakimbizi hao ambao
wana tamaduni na mila tofauti.
kwa
upande wake waziri wa mambo ya ndani mh mathias chikawe amesema tayari serikali
imetenga eneo la migunga wilayani humo
kwa ajili ya kujenga kambi mpya ili kuwahamishia wakimbizi wa burundi na kwamba serikali pamoja na mashirika ya
kimataifa yamelazimika kuongeza huduma katika kipindi hiki ambacho mchakato wa
kuwapa au kutowapa hadhi ya ukimbizi
ukiendelea kwa mujibu wa sheria.
0 comments:
Post a Comment