Uamuzi wa kocha huyo ni kama
amekumbuka shuka asubuhi baada ya kuwaita kikosini wachezaji vijana ambao
alitakiwa kuwaita tangu alipopewa kibarua cha kuinoa Stars.
Kamati ya utendaji ya TFF,
iliyokutana mwishoni mwa wiki ilikuja na azimio kwa kocha Nooij kama atashindwa
kuisaidia timu hiyo kufuzu Chan 2016, kibarua chake kitafikia mwisho.
Pia, kamati ya ufundi wa TFF
ilipewa jukumu la kuangalia kocha mwingine endapo Mdachi huyo atashindwa
kufikia malengo ya kufuzu Chan 2016.
Kutokana na presha hiyo,
Kocha Nooij jana alitangaza kikosi cha wachezaji 16, huku akiwaita kwa mara ya
kwanza wachezaji Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Jonas Mkude (Simba),
Mudathir Yahya, (Azam), Rashid Mandawa, (Kagera Sugar) na Malimi Busungu
(Mgambo JKT).
Kuitwaa kwa wachezaj hao
kunatokana na shinikizo la wadau waliohoji uteuzi wa kikosi cha Taifa Stars
kilichoshiriki mashindano ya Kombe la Cosafa na kutolewa raundi ya kwanza baada
ya kufungwa mechi tatu.
Mjadala mkubwa ulikuwa ni
kuachwa kwa kiungo wa Simba, Mkude wanahabari wengi walihoji kwa nini mchezaji
huyo ameachwa, lakini kocha Nooij alijibu Tanzania ina wachezaji zaidi ya 300,
Mkude ni nani. Mbali ya kiungo huyo, pia kuachwa kwa mshambuliaji Mandawa wa
Kagera Sugar na Busungu wa Mgambo JKT kulizua mjadala kutokana na uwezo
waliouonyesha katika Ligi Kuu msimu uliomalizika kulinganisha na John Bocco
ambaye ndiye kwanza amerejea kutoka bechi alipokuwa majeruhi.
Hata hivyo, ni kama Nooij
ameutua mzigo na lawama alizobebeshwa baada ya kuwachagulia Watanzania
wachezaji wanaowataka watakaoungana na aliowaita yeye mara ya kwanza kwa ajili
maandalizi ya kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Africa (Afcon) na zile za kufuzu
kwa wachezaji wa ndani(CHAN).
Wachezaji hao wataingia
kambini leo kwa ajili ya kupimwa afya zao na kujua maandeleo yao kabla ya
kuwajumisha katika kikosi cha pamoja kitakachokua kwenye maandalizi ya mchezo
dhidi ya Misri. Nooij amewajumuisha kikosini wachezaji Mohamed Hussein, Peter
Manyika, Jonas Mkude (wote Simba), Juma Abdul (Yanga), Mudathir Yahya, Kelvin
Friday (wote Azam), Rashid Mandawa, Atupele Green (Kagera Sugar), Malimi
Busungu (Mgambo JKT) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).Wengine ni Nadir
Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela (Yanga), Frank Domayo, Aishi Manula (Azam),
Haroun Chanongo (Stand United), Hassan Isihaka (Simba), ambao walikuwapo katika
kikosi cha awali cha Nooij, lakini hawakusafiri kwenda Afrika Kusini
kutokana na kuwa majeruhi.
Ofisa Habari wa Shirikisho la
Soka nchini (TFF), Baraka Kizuguto alisema timu hiyo itaanza kambi rasmi Juni
Mosi kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri ugenini, huku wachezaji wanaocheza soka
la kulipwa TP Mazembe, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wakitarajiwa kujumuika
na wenzao siku hiyo.
Alisema kabla ya kwenda
Misri, Stars itaweka kambi Addis Ababa Ethiopia kwa wiki moja kuanzia Juni 4,
kabla ya kuelekea kwenye mchezo huo.
Kizuguto alisema Juni 20,
Taifa Stars itakuwa wenyeji wa Uganda kwenye Uwanja wa Aman Zanzibar katika
mchezo wa kuwania kufuzu kwa Chan 2016, nchini Rwanda 2016 na mchezo wa
marudiano kufanyika baada ya wiki mbili nchini Uganda.


0 comments:
Post a Comment