Kwa mujibu wa shirika la habari la UINGEREZA BBC mtu aliyeshuhudia tukio hilo amesema polisi walifyatua risasi na kisha akaona miili ya watu wawili ikibebwa.
Polisi wamekanusha kuua waandamanaji na badala yake wamesema kuwa askari wake 15 wamejeruhiwa kwa bomu la kurushwa kwa mkono.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani JOHN KERRY amemshauri rais NKURUZIZA kuachana na mpango wake wa kugombea tena urais.
Shirika la misaada la Msalaba Mwekundu limesma watu 12 wameuawa tangu kuanza kwa maandamano hayo Aprili 26 baada ya NKURUZIZA kuidhinishwa na chama chake cha CNDD-FDD kugombea tena urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Mwezi June.
0 comments:
Post a Comment