Image
Image

Mgomo wa madereva wa Dala dala na Mabasi unaoshinikiza kilio chao kwa serikali kwanini unachukua muda kutatuliwa na kuathiri shughuli za watu?.


Nchini Tanzania kwa siku ya pili hivi leo imetikiswa na mgomo wa Madereva wa Mabasi na Daladala kwa kuto safirisha abiria kutoka sehemu moja hadi nyingine hali ambayo imewafanya abiria kuonekana wakihaha huku na kule kutafuta usafiri lakini bado jambo ambalo limefanya watu kutembea kwa mguu kutoka umbali mrefu kutokana na kipato kutokidhi haja ya kukodi Piki piki ya Miguu mitatu(BAJAJI) ama Teksi ambao ndio umekuwa usafiri mkuu jijini dar es salaam na mikoa jirani.
Mgomo huo ukiingia siku ya pili hivi leo umeanza kuonyesha taswira mbili tofauti na jana ambapo leo Mabasi yameonekana kuamriwa kusafirisha abiria huku kukiwa na ulinzi mkali katika baadhi ya mikoa ikiwemo Dar es Salaam,ambapo Basi la Shabiby na Dar express zimeonekana zikifanya safari chini ya ulinzi mkali wa polisi na huko arusha napo abiria waliokuwa wamekwama mkoani mkoani humo tokea jana kutokana na mgomo wa mabasi wameendelea na safari zao  leo hii baada ya jeshi la polisi kudhibiti vikundi vya watu waliokuwa wanatishia kuwashambulia madereva  waliokuwa tayari kuendelea na kazi.

Hata hivyo baada ya mgomo kutikisa bila mafanikio yeyote ya upande wa serikali kuzungumzia mgomo huo licha ya taarifa kuwepo kuwa Waziri mkuu Mh.Pinda aliwaagiza viongozi wa Madereva hao waende ofisini wakayazungumze lakini Madereva waliwakataza viongozi wao kutokwenda kuonana na waziri Pinda kwa madai kuwa endapo watawaruhusu kwenda kuonana na waziri mkuu huenda zikaingizwa siasa na hoja walizo nazo wanzohitaji zitatuliwa zikaishia juu kwa juu bila kutatuliwa.

Hata hivyo Wizara ya Uchukuzi ilitangaza jana kuwa Waziri Mkuu MIZENGO PINDA alikuwa ameunda kamati ya watu 13 ambayo itakuwa kamati ya kudumu ya kushughulikia mambo yote ya madereva kwa kuanzia na mgomo wa sasa.

Katika mgomo huo sasa imemladhimu kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha Bw.Harson Mwakyoma kutoa amri chini ya usimamizi mkuu wa kikosi chake ili mabasi jijini humo kupeleka abiria ambao walikwama tokea jana kufuatia mgomo huu ambao ukomo wake bado kitandawili na kuamuru mabasi yaanze safari nahivyo kuanza safari hivi leo kutoka Arusha kwenda mikoa mingine ikiwemo Dar es Salaam na hivyo kusema kama jeshi la polisi wamejipanga  kikamilifu kukabiliana na watu wanaotishia kuwashambulia madereva na abiria kwa kuweka askari  maeneo yote korofi na pia kuyasindikiza mabasi hadi mwisho wa safari.

Aidha kamanda Mwakyoma pia amewaasa madereva kuthamini kazi zao na kuepuka kutumiwa na baadhi  ya watu wenye malengo ya kuwagombanisha na serikali na pia na wamiliki wa mabasi.

Katika hili baadi ya wadau wameendelea kuitaka serikali kuangalia upya namna ya kuweka utaratibu endelevu  wa kuwawezesha  madevera kufanya kazi zao kwa salama na amani bila kuonewa na  kuingiliwa na watu ama idara nyingine.

Aidha mgomo huu ambao unaendelea kila uchao unaonekana kugubikwa na sinto fahamu huku sura ya itikadi za siasa ikionekana kuingizwa ndani ya mgomo huu ambao tayari umeshaanza kuathiri mamia ya watanzania,haswa wale ambao ni hoe hahe hawana kipato cha kutosha na wanaotegemea usafiri huo wa dala dala ili kwenda kufanya shughuli zao za kila siku za kujiingizia kipato.

Mgomo umeathiri makundi mbali mbali katika skta zao,mgomo huu ulipoanza umedondokea siku ambayo wanafunzi wa kidato cha sita wanaanza kufanya mitihani yao ya mwisho hivyo kuonekana kuwaathiri huku wakiwa na msongo wa mawazo wa namna gani watafika katika chumba cha mtihani huku magari yakiwa hayapo kutokana na mgomo,wenye uwezo ndio walipata bahati ya kuwahi mitihani na masomo ya kawaida ila wasio na kipato cha kutosha ilikuwa ni tabu kwao hali ambayo hapo baadae serikali huenda ikabeba lawama kwa kuonekana kufumbia macho mgomo huu yatakapo tangazwa matokeo ya mtihani yakionyesha kiwango cha ufaulu kimeshuka lawama zitatupwa moja kwa moja kwa serikali kwamba hadi hivi nikutokana na na Mgomo ulioanza May 4 hadi 5 au zaidi ndio ulioathiri sekta ya elimu.

Hivi kunaswali la kujiuliza kuwa mgomo huu umekubikwa na nini nyuma ya pazia kwakuwa baada ya mgomo wa awali uliopata suluhisho Ijumaa,10 Aprili 2015 21:44.Serikali ya Tanzania ilazimika kutengua uamzi wake wa kutaka madereva wa mabasi ya abiria nchini humo,kurudi mafunzoni kila baada ya miaka mitatu,baada ya madereva hao kufanya mgomo wa kutoa huduma za usafirishaji nchi nzima.Katika mgomo huo polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kutuliza ghasia zilizosababishwa na madereva hao.

Kwa kipindi hiki cha May 3 nakuendelea mabomu ya machozi hayakupewa nafasi kabisa ambapo mgomo huo uliendelea huku viongozi wa madereva hao wakiwa wanaisihi serikali kusikiliza kiliochao na kutoa ufafanuzi ili kutatua mgomo huu ambao hauoneshi taswira nzuri kwa mataifa ya wenzetu na nchi jirani ila jambo kuu ni kuketi na kuzungumza lugha moja kuliko serikali kuzungumza na wamiliki wa mabasi pekee na kuwaacha wahusika wanaoumia.

Nimatumaini yangu kwamba suluhisho la mgogoro ni maridhiano yenye mrengo wa kutatua tatizo ama matatizo yanayo wakabili watu mbali mbali kuliko nchi kila uchao unatoka mgomo unaingia mgogoro wa wafugaji na wakulima,ubadhirifu wa fedha kwenye akaunti mbali mbali Escrow na mengine mengi,hivyo lugha moja inajenga nchi na maridhiano ndio yanayo tutoa hapa tulipo katika lindi la umasikini na kutupeleka mbele zaidi.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Afrika.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment