Image
Image

Wachimbaji haramu wa madini ya almasi maarufu kama WAHABESHI zaidi ya miamoja wamevamia mgodi wa madini ya almasi MWADUI SHINYANGA.


                                          Picha na maktaba yetu.
Wachimbaji haramu wa madini ya almasi maarufu kama WAHABESHI wanao kadiriwa kuwa zaidi ya miamoja ,wamevamia ndani ya mgodi wa madini ya almasi  MWADUI SHINYANGA kwa lengo la kupora mchanga unaodhaniwa kuwa na almasi na kusababisha mauaji ya mchimbaji mdogo mmoja na askari mmoja wa mgodi huo kujeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa jeshi la polisi mkoani shinyanga JUSTUS KAMUGISHA tukio hilo limetokea tarehe 4 majira ya saa 7 mchana  ambapo baada ya wachimbaji hao kuvamia ndani ya mgodi huo walisababisha mapigano makubwa hali iliyosababisha machafuko makubwa katika eneo hilo.
Aidha kamanda kamugisha amesema vita hivyo ambavyo vilihusisha silaha za jadi na za moto ambapo wachimbaji hao walirusha jiwe kwa kutumia kombeo na kumvunja kidole cha mkono wa kushoto ambaye ni mlinzi wa kampuni ya zenith securty na kupelekea mapigano makubwa yaliyosababisha  mauaji ya kijana huyo.
Kamugisha alimtaja mchimbaji aliyeuawa katika mapigano hayo kuwa ni michael shija miaka (28) ambaye alipigwa na kitu chenye ncha kali chini ya  kwapa la mkono wa kulia na kusababisha kifo chake na  mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hosptitali ya mkoa wa shinyanga.
Pia kamanda alimtaja mlinzi wa kampuni ya ulinzi zenith security aliyrjeruhiwa kuwa ni ligwa saida miaka (29), ambaye alipigwa jiwe na wachimbaji hao na kusababishiwa majeraha kwenye mwili wake ambaye naye anapa amelazwa katika hosptitali ya mkoa wa shinyanga.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment