Image
Image

News Alert: Awamu ya Tatu yenye jumla ya Watanzania 39 kutoka Yemen wanatarajiwa kuwasili nchini


Awamu ya Tatu yenye jumla ya Watanzania 39 kutoka Yemen wanatarajiwa kuwasili nchini tarehe 06 Mei, 2015 ikiwa ni jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwarejesha nyumbani kufuatia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini humo.
Watanzania hao wakiwemo Wanafunzi watawasili nchini kwa Ndege ya Shirika la Qatar namba QR 1349 majira ya saa 1.55 (saa moja) asubuhi.

Kurejea kwa Watanzania hao kutafanya jumla ya Watanzania waliorejea kutoka Yemen hadi hivi sasa kuwa 62 kati ya   Watanzania 69 waliojiandikisha kurudi  huku jitihada za kuwaandikisha wengine zikiendelea kufanywa na Ubalozi wa Tanzania nchini Oman.

Awamu ya kwanza ya Watanzania waliorejea ilihusisha familia ya watu watano huku awamu ya pili ilikuwa na Watanzania 18.

Itakumbukwa kuwa, hivi karibuni Serikali kupitia Waziri wa Mambo  ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe ilitangaza kuwarejesha nchini Watanzania waliopo Yemen kufuatia machafuko yanayoendelea nchini humo.

IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.

05 MEI, 2015
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment