Wakazi wa vijiji 10 vilivyopo katika kata
tofauti wilayani kilindi wanahangaikia huduma ya maji huku wengine
wakitembea umbali mrefu kufuatia kusimama kwa mradi wa maji wa shilingi
bilioni 4.5 unaoratibiwa na mkopo wa benki ya dunia katika vijiji 25
vilivyopo wilayani humo.
Wakizungumza katika kijiji cha kileguru,wakazi wa
vijiji vinne viliyopo kata ya kilwa wilayani kilindi wamesema baadhi ya watu
wamekuwa wakisumbuliwa na homa za matumbo kwa sababu ya matumizi ya maji
yasiyokuwa salama katika maeneo yao.
Akielezea hatua hiyo mhandisi wa maji wilayani
kilindi eng'renatusi gua amesema mradi wa maji umesimama kutokana na ukosefu wa
fedha na wakandarasi waliowekeana mkataba na serikali wamesitisha shughuli
za ujenzi katika vijiji hivyo hadi hali ya fedha itakaporuhusu.
0 comments:
Post a Comment