Kituo cha kuchakata Gesi cha madimba kilichopo
wilaya ya Mtwara vijijini Mkoani Mtwara kimekamilika kwa asilimia 97, baada ya
miezi miwili kitazalisha umeme wa MEGA WATS 350 kwa kuanzia, ambao utaongezwa
kwenye Gredi ya taifa ambayo kwa sasa ina MEGAWAT 1300.
Kauli hiyo imekuja baada ya mkurugenzi mkuu wa
shirika la maendeleo ya Petroli nchini TPDC James Mataragio na timu yake
kutembelea kituo hicho na kujionea sehemu kubwa ya mradi huo ukiwa umekamilika,
huku akisisitiza gesi hiyo itasafirishwa katika kituo cha kinyerezi na ubungo.
Amesema kituo cha Kinyerezi kinatarajiwa kufua umeme
wa MEGAWATT 156 kwa kuanzia wakati kituo cha ubungo
kinatarajiwa kufua umeme wa MEGAWATT 200 ambao utaongezwa kwenye Gridi ya taifa
yenye umeme wa MEGA WAT 1300 kwa sasa.
Akizungumzia ulinzi wa bomba la Gesi linalokwenda
Dar es Salaam ambalo limekamilika kwa asilimia 100 Mataragio amesema TPDC
tayari imetoa elimu ya kutosha kwa wananchi wanaopitiwa na bomba hilo kuwa
walinzi sambamba na kuvitumia vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha bomba
hilo linakuwa salama wakati wote.
Mradi huo ulianza mwaka 2013 umegharimu dola za
kimarekani bilioni 1.2, kwa sasa utaendeshwa na wataalamu wa kigeni kwa
kushirikiana na watanzania wachache waliopata mafunzo kutoka china na baada ya
mwaka mmoja utasimamiwa na watanzania,na utatoa ajira kwa wananchi wenye elimu
ya kawaida.
Kituo hicho kimejengwa na mataifa matano, wataalamu
toka china, marekani, South Afrika, Austrelia, na Uingereza.
0 comments:
Post a Comment