Walioshuhudia wanasema kuwa mlipuaji wa kujitolea mhanga aliendesha gari lake moja kwa moja hadi kwenye lango kuu la kituo hicho .
Kituo hicho kiko katika eneo la Leego, barabara kuu inayounganisha mji mku wa Mogadishu na Baidoa.
Wanamgambo hao wa Al shabaab wamesema wameteka kituo hicho, lakini wanajeshi wa muungano wa Afrika nchini humo , AMISON wamekanusha madai hayo.
AMISOM inasema kuwa wanajeshi wake wanaendelea kukabiliana na wanamgambo hao wa kiislamu.
Kundi la al shabaab limeimarisha mashambulio ya kigaidi tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa mfungo wa ramadan.
Kituo hicho kinaendeshwa na wanajeshi kutoka Burundi chini ya mwavuli wa (Amisom).
Jeshi hilo linazaidi ya askari 20,000 kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
0 comments:
Post a Comment