Balozi Amina ambaye ni Balozi wa Kudumu wa Umoja wa
Afrika (AU) nchini Marekani alitoa kauli hiyo jana katika Kipindi cha Funguka’,
kilichoanza kurushwa na Azam TV, baada ya kuulizwa swali na mwendeshaji wa
kipindi, Tido Mhando.
Mwanadiplomasia huyo alitoa jibu hilo alipoulizwa
kwa nini hakutaka kugombea tena urais wa Zanzibar wakati alionyesha nia ya
kuongoza Zanzibar mwaka 2000.
Akijibu swali hilo alisema, “Kwa sasa tunapita
kwenye kipindi kigumu na mie ninakiri kwamba, Rais tuliyenaye anajitahidi, kwa
sababu Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ni mpya, hajamaliza muda wake na
tunaona jinsi alivyoongoza,” alisema.
Alisema ni vyema Dk Shein akapewa nafasi ya
kuendelea kuongoza licha ya kuwapo kwa wanachama wanaotamani nafasi hiyo.
Mwombaji huyo wa urais wa muungano kupitia CCM
alisema Wazanzibari wengi wameonyesha nia ya kumwamini Dk Shein.
Kuhusu SUK na hali ya kutofautiana kisiasa, Balozi
Ali alisema umoja huo ulikuwa ni majaribio ambao umeonyesha unafuu mkubwa
katika mahusiano ya Wazanzibari, hivyo serikali hiyo haitakiwi kuvunjwa.
Kuhusu
Muungano
Akizungumzia mahusiano ya muungano kati ya Tanzania
Bara na Zanzibar, Balozi Ali alisema changamoto kubwa iliyopo ni kukosekana kwa
utekelezaji wa mambo yanayojadiliwa ndani ya vikao vya serikali hizo mbili.
“Mambo yalijadiliwa na kukubaliwa lakini kila jambo
lilionekana kama ni nyeti au la kisiasa au haliwezekani, matokeo yake mambo
yamekuwa ni mengi mpaka kufikia hatua ya kufanyia mapitio ya katiba,” alisema
na kuongeza:
“Mambo yanayowaumiza Zanzibar ni masuala ya uchumi
na upande mwingine ni masuala ya kisiasa na Itifaki. Ilikuwa wakati mwafaka wa
kuyafanyia maboresho, ukiangalia katika mapendekezo ya Katiba kama kuna mambo
ambayo yangefanyiwa kazi, yangeweza kuleta nafuu katika mfumo wetu,” alisema.
Alipoulizwa ni kwa jinsi gani ataondoa kero na
changamoto za muungano huo, mgombea huyo alisema Muungano huo haukuwa na kero
ila zilikuwa changamoto tu ambazo zimebadilika kuwa kero baada ya kuchukua muda
mrefu bila kushughulikia.
0 comments:
Post a Comment