Image
Image

Kamati ya mpito ya Nigeria yamshauri MUHAMMADU BUHARI kuondoa ruzuku ya mafuta


Kamati ya mpito ya Nigeria imemshauri rais mpya wa nchi hiyo  Bwana MUHAMMADU BUHARI kuondoa  ruzuku ya mafuta na kutaifisha vinu vinne vya kusafishia mafuta nchini humo.
Nigeria ambayo ni mtoaji mkubwa wa mafuta barani Afrika na ye nye uchumi mkubwa inatoa ruzuku  kubwa ya mafuta ya taa na kutegemea mafuta mengi yaliyosafishwa kutoka nje kwa matumizi ya  ndani  kutokana na uduni wa mitambo ya kusafishia mafuta nchini humo.
Ruzuku ya mafuta imebainika na kudaiwa kugharimu zaidi ya dol a bilioni sita za ubadhirifu na  kudhihirisha kuongezeka gharama kubwa kwa serikali na kwamba  kutaifishwa kwa vinu vya mafuta  kutaiwezesha serikali iache kupoteza fedha za matengenezo makubwa ya kila mwaka.
Miaka mitatu iliyopita Nigeria ilijaribu kuondoa ruzuku za maf uta na kuongeza maradufu ya bei  yake katika juhudi za kupunguza matumizi ya serikali hatua i liyowakasirisha raia wake kwani  walioona bei nafuu ilikuwa ndiyo gawio pekee kwao kwa kuishi katika nchi tajiri kwa mafuta.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment