Ugiriki inakabiliwa na wakati
mgumu wakati viongozi wa Ulaya wakiwa wanakutana Brussels,Ubelgiji kwa kikao cha dharura kutatua mgogoro wa
madeni ya nchi hiyo katika juhudi za kuinasua kiuchumi.
Hapo jana Waziri Mkuu wa Ugiriki
Bwana ALEXIS TSIPRAS alitan gaza mapendekezo mapya kujaribu kuzuia nchi yake isishindwe kulipa mkopo wa
Shirika la Fedha l a Kimataifa IMF wa YURO BILIONI 1.1.
Afisa mmoja wa Ulaya alisema
mapendekezo hayo yalikuwa na ahadi
nyingi wakati Ugiriki inatakiwa
lazima ilipe deni hilo kufikia mwishoni mwa mwezi huu au kuwa hata rini
kuondolewa kwenye matumizi ya sarafu ya
YURO na pia uanachama wa Umoja wa Ulaya.
Mazungumzo yamekwama kwa miezi
mitano baada ya Tume ya Ulaya, Shirik a la Fedha la Kimataifa IMF na Benki Kuu ya Ulaya kukataa kuipa Ugiriki
YURO bilioni 7.2 za ku inusuru kiuchumi nchi hiyo hadi ifanye mageuzi wanayotaka ifanye ikiwa
pamoja na kubana matumizi.
0 comments:
Post a Comment