BAADA
ya kumtimua Kocha Mkuu wa timu ya taifa (Taifa Stars), Mart Nooij
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inafikiria kuwakabidhi
kikosi hicho makocha wazawa Boniface Mkwasa au Hemed Moroco.
Kwa
mujibu wa habari kutoka ndani ya kikao cha Kamati ya Utendaji
kilichokutana juzi mjini Zanzibar ambacho kilifikia kumfukuza, Nooij
zimeeleza kuwa baada ya kuafikiana kumuondoa kocha huyo baadhi ya
wajumbe walipendekeza majina hayo mawili.
"Baada ya kukubaliana
kumfukuza kocha Nooij, baadhi ya wajumbe walipendekeza majina ya makocha
wazawa Boniface Mkwasa na Hemes Moroco ambao wana uzoefu na kazi hiyo,"
kilieleza chanzo cha habari hizi.
Hata hivyo habari hizo zinaeleza
kuwa walikubaliana kutoa msimamo kuhusu uteuzi wa makocha hao, baada ya
kuwasikiliza kwanza wenyewe kuhusiana na suala hilo.
Chanzo hicho
kilieleza kuwa makocha hao hadi jana wangekuwa wamejulishwa kuhusiana na
uteuzi wao, kila kitu kitawekwa hadharani wiki hii.
Akizungumzia
fununu hizo, Mkwasa alisema tetesi hizo za kukaimu nafasi hiyo ya Nooij,
ameshazisikia lakini anasubiri taarifa rasmi ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF).
Mkwasa alisema akiwa kama kocha wa soka hawezi
kukataa jukumu la kuifunza timu ya taifa, lakini cha msingi ni kupata
barua rasmi kutoka TFF.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment