Image
Image

Boko Haram wawauwa watu wapatao 40 wakiwemo wanawake na watoto Niger.


Watu wapatao 40 wakiwemo wanawake na watoto wameuawa Niger na watu  wenye silaha wanaosadikiwa kuwa  wapiganaji wa Nigeria wa kikundi cha Boko Haram.
Taarifa zinasema mauaji hayo yametokea katika vijiji viwili tofauti na shambulio hilo ni la pili kwa wapiganaji wa Boko Haram huko Niger baada ya lile la mwezi  Aprili mwaka huu ambao watu 58 waliuawa.
Niger ni miongoni mwa nchi nne jirani zinazoongozwa na Niger ambazo  zimeunda kikosi cha pamoja cha  kupambana na kikundi hicho cha Boko Haram ambacho mashambulio ya ke pia yameingia nchi jirani na Nigeria.
Mapema wiki hii mashambulio ya kujitoa mhanga yaliyofanywa na w anawake wawili wa kikundi hicho  katika mji mkuu wa Chad, N'Djamena yaliuawa watu 24 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment