Rais
UHURU KENYATTA wa Kenya amesema serikali yake itarejesha leseni kwa kampuni 13 za uhamishaji fedha zilizodaiwa kuangukia mikononi mwa
wapiganaji wa Somalia wa kikundi cha al-Shabaab.
Kutokana
na madai hayo makampuni hayo yalipigwa marufuku na kunyang' wa leseni baada ya
shambulio la maafa kwenye Chuo Kikuu cha
Garis mwezi Aprili mwaka huu am bapo watu wapatao 150 wengi wao wanafunzi waliuawa.
Mauaji
kwenye chuo hicho kilichoko kilomita 200 kutoka mpakani na Somalia kulileta shinikizo kwa Rais KENYATTA kukabiliana na wapiganaji hao
ambapo katika miaka miwili iliyopita
wameua zaidi ya watu 400 huko Kenya.
Makundi
ya haki za binadamu yanasema kupigwa marufuku kwa makamp uni hayo ya uhamishaji
wa fedha kumeleta athari kubwa kwa jamii
ya Wasomalia wanaoletewa fedha na nd ugu zao wanaofanya kazi nchi za nje.
0 comments:
Post a Comment