Kumekuwa
na taarifa za kuweko watu wanaotaka kushambulia Burundi hali iliyozidisha kasi
ya watu wanaotoroka nchi.
Chama tawala nchini Burundi kinaomba uchuguzi ufanyike
juu ya taarifa za kuwepo mafunzo ya kijeshi kwa wakimbizi wa Burundi
waliokimbilia katika nchi jirani za Rwanda Tanzania na Jamuhuri ya kidemokrasia
ya Kongo kwa nia ya kuivamia Burundi na kuvuruga uchaguzi mkuu nchini humo.
Kumekuwa na taarifa za kuweko watu wanaotaka
kushambulia Burundi hali iliyozidisha kasi ya watu wanaotoroka nchi.
Hayo yalikuwa katika tangazo lenye ukurasa 9 lililotolewa
Alhamisi usiku na chama hicho.
Tangazo hilo lina lengo la kuelezea msimamo wa
chama hicho kuhusu maamuzi ya mkutano wa umoja wa afrika uliofanyika jijini
Johanesbourg nchini Afrika ya kusini.
Miomgoni mwa maamuzi ya mkutano huo ni kuwata wadau wa
uchaguzi wa Burundi warejee kwenye meza ya mazungumzo.Umoja wa afrika ulieleza
kuwa utawatuma watalaam wa kijeshi ambao watajihusisha na kuwapokonya silaha
watu wanazozimiliki kinyume cha sheria na kuomba mazungumzo kwa ajili ya
kumaliza mgogoro huu wa kisiasa yaanze upya.
Wakati huo huo, Mwanasheria aliyeteuliwa kuziba nafasi
ya kurejelea mjumbe wa korti ya katiba aliyetoroka nchi baada ya kukataa
kuidhinisha rais wa Burundi kuwa ana haki ya kugombea muhula wa tatu amekula
kiapo hii leo mbele ya rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. Bwana Benoit
SIMBARAKIYE pamoja na mjumbe mwingine wa korti hiyo wameahidi kufanya kazi bila
kuegamia upande wowote na kuheshimu makubaliano ya umoja wa warundi.
0 comments:
Post a Comment