Watu 23 wamekufa na wengine 34
wamejeruhiwa, wanne kati yao hali zao ni mbaya,kutokana na ajali iliyotokea
katika eneo la Kinyalamambo, Mafinga Mkoani iliyohusisha basi dogo aina ya
Coaster na lori la mizigo.
Magari hayo yaligongana kwenye
barabara kuu ya Iringa-Njombe na chanzo cha ajali hiyo ni mwendo-kasi.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Iringa, PUDENCIANA PROTAS amesema
baso hilo lilikuwalikitokea Iringa kwenda Njombe na kwamba majeruhi 30
wamefahamika kwa vile wanaweza kuzungumza na hali zao zinaendelea vizuri.
Amesema miongoni mwa waliokufa ni
dereva wa lori na wengine 22 ni kutoka
kwenye basi na miili imehifadhiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mafinga na
maiti 12 wametambuliwa na waliobaki hawajatambuliwa.
0 comments:
Post a Comment