Vijiji hivyo vya kata za
Bugarama,Bulyanhulu na Mwingiro vyenye zaidi ya wakazi 47,000, wananchi
wamekuwa wakiwaomba bila mafanikio viongozi mbalimbali kushughulikia
tatizo hilo ambalo limekuwa ni tishio kubwa kwa usalama wa afya zao.
Baadhi
ya wananchi wa kata za Bugarama na Bulyanhulu wamesema bado tatizo hilo la
ukosefu wa huduma bora za afya limekuwa likiwasumbua kwa kiasi kikubwa licha
ya kuwepo kwa zahanati moja ambayo haikidhi mahitaji hususani ya ongezeko la
watu huku kinamama wajawazito wakipata usumbufu mkubwa katika kutafuta huduma
za upasuaji zinapohitajika.
Aidha katika kusaidia
kukabiliana na hali hiyo kampuni ya ACACIA inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu
imeamua kujenga kituo kikubwa cha afya kinachogharimu zaidi ya shilingi milioni
800 kwa awamu ya kwanza ikiwa ni moja ya muendelezo wa kusaidia huduma za
kijamii kwa vijiji vinavyouzunguuka mgodi huo wa dhahabu ambapo pia kampuni
hiyo ya acacia mbali ya kuchangia pato kubwa serikalini wastani wa dola za
kimarekani milioni 62 kwa mwaka lakin imekuwa ikishiriki vema miradi ya ujirani
mwema katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii katika sekta za
elimu,kilimo na maji.
0 comments:
Post a Comment