Taarifa ambazo zimetufikia punde zinaeleza kuwa kiongozi mkuu wa
waislamu nchini Tanzania Mufti Issa Bin Shaaban Simba amefariki dunia.
Hakika ni majonzi na pigo kubwa
kwa Waislam na watanzania kwa ujumla.
Chanzo kuhusu kifo chake bado hatujafamu lakini tumejaribu
kumtafuta
Sheikh wa mkoa wa Dar es
Salaam, Pichani hapo Alhad Musa Salum kuweza luweka
bayana ukweli juu ya taarifa hizi zinazo samba kwa wakati huu kupitia mitandao
ya kijamii,lakini simu yake imekuwa iko bize sana ambapo bado tunafanya juhudi
hadi tumpate kujua ukweli wa kifo cha Mufti Simba.
Amezaliwa Shaaban na ameondoka ndani ya mwezi wa Shaaban,
Innalilah wainailah Rajiun.
Innalilah wainailah Rajiun.
Mwenyezi mungu ampe kauli thabiti na amjaalie pepo ya kheri na
kumsamehe madhambi yake.
Dar es Salaam.
Dar es Salaam.
Sheikh Mkuu wa Tanzania,
Mufti ISSA SHAABAN SIMBA amefariki dunia
leo asubuhi katika Hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,
ALHADI MUSSA SALUM amethibitisha kifo hicho alipozungumza na Radio One Stereo
na kusema maelezo zaidi yatatolewa
baadaye.
Habari zinasema mwili wa marehemu
umeondolewa kutoka hospitalini hapo na kupelekwa Hospitli kuu ya jeshi Lugalo
na wakati mipango ya mazishi inafanywa.Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi.
Taarifa wapi atakapo zikwa Muft Shaban Simba.
Taarifa wapi atakapo zikwa Muft Shaban Simba.
Shekhe wa Dar es salaam Alhad
Musa Salum amesema kuwa Shekhe mkuu mufti wa Tanzania Isaa Bin Shaaban Simba
anatarajiwa kuagwa kesho saa nne asubuhi katika ofisi za bakwata makao makuu
kinondoni jijini Dar es Salaam na kusomewa dua maalum majira ya saa tisa mchana
kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani shinyanga kwa maziko
Marehemu mufti simba amefariki
asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam katika hospitali ya TMJ wakati akipatiwa
matibau
0 comments:
Post a Comment