VVyama 17 vya upinzani nchini Burundi vimesema havina tena imani na mjube
maalumu wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Maziwa Makuu, Said
Djinnit, na kuomba mpatanishi mpya katika Umoja wa Mataifa.
Vyama vya upinzani nchini Burundi vimemtuhumu
mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa maziwa makuu Said Djinnit
ambae ni mpatanishi wa mgogoro wakisiasa uliopo kwa kuegemea upande mmoja na
kuomba kuteuliwa kwa mpatanishi mwingine katika mazungumzo na serikali ya rais
Pierre Nkurunziza.
Vyama hivyo vinamkosoa Djinnit kuwasilisha
ripoti yake kwa marais wa nchi za jumuiya ya Afrika mashariki mjini Dar es
Salaam juma lililopita bila ya kuwashirikisha kwa kile kilichoandikwa katika
ripoti hiyo.
Hata hivyo Said Djinnit amehakikisha kuwa
bado hajaona waraka huo uliyowasilishwa na upinzani kwa Katibu mkuu wa Umoja wa
Mataifa.
Wakati hayo yakijiri, naibu waziri wa mambo
ya nje wa Marekani mwenye dhamana ya Demokrasia na Haki za Binadamu, Tom
Malinowski aliyemaliza ziara yake nchini Burundi amemtaka rais Pierre
Nkurunziza kutogombea muhula wa tatu jambo ambalo amesema ni kinyume na
makubaliano ya Arusha.
Sanjari na hayo, Umoja wa Mataifa umetoa wito
Alhamisi wiki hii wa kuwapokonya silaha haraka iwezekanavyo vijana wa chama
tawala maarufu kama Imbonerakure ili kuruhusu maandalizi ya uchaguzi ulio huru,
wa haki na wa amani nchini Burundi. Kutangaza kuwania muhula wa 3 kwa rais
Nkurunziza kumeendelea kuzua ghasia nchini humo ambapo watu zaidi ya 30
wamepoteza maisha katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu.
0 comments:
Post a Comment