Akizungumza na waandishi wa habari mjini New
York, msemaji wa Katibu Mkuu, Stephane Dujarric, amesema kuwa Mkuu wa ujumbe
huo, Babacar Gaye alianzisha uchunguzi mara moja baada ya kupokea taarifa hizo,
na kujulisha mamlaka za CAR.
"Amekariri kuwa kulingana na sera ya
Umoja wa Mataifa ya kupinga kabisa uhalifu wa kingono, hatua zimechukuliwa za
kumlinda mwathiriwa, ambaye pia amehudumiwa ipasavyo. Umoja wa Mataifa pia
umeiomba serikali anakotoka askari huyo kuanzisha uchunguzi mara moja."
Hiki si kisa cha kwanza cha madai ya ukatili
wa kingono unaodaiwa kufanywa na walinda amani dhidi ya watoto nchini Jamhuri
ya Afrika ya Kati. Tayari uchunguzi unaendelea kuhusu madai ya askari wa
Ufaransa kuwanyanyasa watoto kingoni nchini humo.
0 comments:
Post a Comment