KIUNGO
anayefanya majaribio Yanga,Lansana Camara kutoka Sierra Leone amesema
atatumia mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Sports Club Villa ya Uganda
kuonesha uwezo wake na itakuwa kipimo kizuri kwake kama anafaa au la.
Camara kwa sasa yupo katika majaribio na timu ya Yanga kwa ajili ya kusajiliwa kwa msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara.
Uongozi
wa benchi la ufundi wa timu hiyo, chini ya kocha Mholanzi, Hans Pluijm
umempa muda zaidi kiungo huyo mwenye umbo la kiuchezaji ili aoneshe
uwezo wake na kuushawishi uongozi kumsajili.
Camara amenukuliwa akisema kuwa mechi hiyo itakuwa muhimu kwake kuonesha uwezo wake uwanjani.
"Tangu
nimefika nimekuwa nikifanya mazoezi ya viungo, sasa mechi itatoa nafasi
zaidi kuushawishi uongozi kunisajili," alisema Camara.
Camara,
ambaye alikuwa akicheza klabu ya Umea FC inayoshiriki Ligi Daraja la
Kwanza Sweden, alikutana na Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm na kufanya
naye mazungumzo kuelekea ndoto yake ya kutua katika klabu hiyo.
“
Nina furahia mazoezi yangu na mashabiki wengi wanakuja kutuangalia, hii
inatia moyo,” alisema Camara, ambaye anafanya mazoezi na timu hiyo kwa
sasa.
Yanga imeanza mazoezi takriban wiki mbili zilizopita katika
viwanja vya kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu.
Yanga na Villa watavaana Jumamosi Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment