Dodoma.
Bunge limeelezwa kuwa Serikali
imetenga Shilingi BILIONI 1 na Milioni 2
00 katika mwaka 2015/ 20 16 kwa ajili ya
kuboresha huduma ya maji katika mji wa Muheza mkoani Tanga.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu
Waziri wa Maji,AMOS MAKALA alipokuwa akijibu
swali la mbunge wa Muheza,JAMES MTANGI aliyeuliza jiji la Tanga linapata kiasi
gani kwa mapato ya maji kwa mwaka mmoja kutokana na chanzo cha Mto Zigi ambapo
wilaya ya Muheza inaachia maji bila gharama kwa Jiji la Tanga.
MAKALA amesema majadiliano kati ya
serikali na kampuni ya EUROFINSA yanaendelea ili kupata fedha za kutekeleza
mradi mkubwa kwa mji wa Mheza kupitia chanzo cha Mto Zigi.
Na Serikali imeanza kutekeleza
awamu ya tatu ya mradi wa mkongo wa taifa ambapo Dola za
Marekani Milioni 93 NA Laki- 7 na
Shilingi BILIONI 2 zitawekez wa katika ujenzi wa mtandao pamo ja na kituo
mahiri cha kutunzia kumbukumbu kitakachowezesha kumbukumbu kuhifadhiwa hapa
nchni na kurahisisha matumizi ya TEHAMA.
Waziri wa Mawasiliano,Sayansi
na Teknolojia,Profesa MAKAME
MBARAWA amesema hayo alipokuwa a kijibu swali la Mbunge wa Igalula,ATHUMANI
MFUTAKAMBA liyetaka kujua serikali mejipanga vipi kuhakikisha Tanzania inakuwa
kitovu cha mawasiliano Afrika Mashariki kwa ujumla kwa kuongeza biashara na
matumizi ya komputa.
Profesa MBARAWA Amesema kituo
kituo hicho kitakachojengwa kitaruhusu utunzaji wa kumbukumbu hapa nchni pamoja
na nchi jirani zitakazopenda kujiunga na kituo hicho.
0 comments:
Post a Comment