Serikali inawaahidi wananchi wote
kuwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa Oktoba mwaka huu utafanyika kwa mujibu wa
sheria,kanuni na taratibu zilizopo.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu,JENISTA MHAGAMA
ametoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la Mbunge Mtambile ,MASOUD SALIM,kuwa
serikali inawaahidi nini wananchi kwamba
baada ya uchaguzi huo atakayeapishwa ndiye mshindi halisi, na nini
mkakati wa serikali wa kukomesha uvurugaji wa sheria na
ukandamizaji wa demokrasia.
Waziri MHAGAMA amesema Tume ya
Taifa ya Uchaguzi inaendelea na maandalizi ya uchaguzi mkuu ili kuhakikisha
washindi wanapatikana kwa haki na vyama vya siasa vitashiriki katika hatua zote
kuanzia kampeni hadi kutangazwa kwa wagombea.
Kuhusu swala la demokrasia ametoa
wito kwa wadau na wananchi wote kuhakikisha kutojichukulia sheria mikononi au
kujihusisha na vitendo vyo vyote
vinavyokiuka sheria,kanuni na taratibu za uchaguzi ili kudumisha amani na
usalama katika kipindi chote cha uchaguzi mkuu.
0 comments:
Post a Comment