Hayo yameelezwa na mkuu wa kambi
ya wakimbizi Nyarugusu,Wilayani
Kasulu, inayopokea na kuwahifadhi kwa sasa raia hao ku toka Burundi,SOSPETER BOYO,wakati wa
maadhimisho ya siku ya Wa kimbizi
duniani .
Amesema hivi sasa wanapokea kati
ya wastani wa wakimbizi 150 na 200 kwa
siku na wengi wamekuwa wakiingilia kupitia
vijiji mbalimbali vya Mkoa wa Kigoma, na kwamba kutokana na hali
hiyo kambi sasa ina zaidi ya
wakimbizi Laki- moja na Elfu- kumi
wakati Warundi wakiwa Elfu- 57 .
Kwa upande wake Mratibu wa Shirika la Kimataifa linalo shughulikia afya na maji kambini hapo -
OXFAM- Bwana VICENT OTIENO amesema shirika hilo linasaidia
kuongeza huduma ya maji kutokana na miundombinu iliyopo kuwa na uwezo wa
kuhudumia watu wacahache huku wakimbizi wakiomba kujengwa haraka kwa makazi yao
kutokana na msongamano uliopo sasa kuhatarisha afya zao .
0 comments:
Post a Comment