Image
Image

Polisi lamnasa jangili sugu aliyekuwa na meno ya Tembo aliyetoroka baada ya kuhukumiwa Mkoani Simiyu.


Jeshi la polisi mkoani simiyu kwa kushirikiana na kikosi maalum cha askari wa hifadhi ya taifa ya serengeti  wamefanikiwa  kumkamata mtuhumiwa wa ujangili  Bw.Madeni Nindwa mkazi wa kijiji cha mwalukonge wilayani busega aliyekamatwa na meno ya tembo yenye thamani shilingi milioni 17,baada ya kutoroka na hatimaye  kukamatwa katika kijiji cha makomero wilayani igunga alikokuwa amejificha.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kaimu kamanda wa polisi mkoa wa simiyu SSP JONATHAN SHANA amesema kuwa kesi ya jangili huyo ilifunguliwa ,katika mahakama ya wilaya ya magu  EC2/2014 mbele ya hakimu Josephati Masige ambapo iliendeshwa siku tatu mfulilizo  kuanzia,desemba 2 hadi  5,2014 na kumalizika kusikilizwa na mtuhumiwa alijitetea januari,8,2015 na kubaki hukumu dhidi yake.
Amesema katika mazingira ya kutatanisha mtuhumiwa januari 13 mwaka huu, alitolewa gerezani kwa hati ya mahakama iliyosainiwa na hakimu aliyekuwa akiisikiliza kesi hiyo bila kuwepo kwa wakili mwandamizi mfawidhi wa wa serikali .
SHANA amesema jalada la uchunguzi limefunguliwa kupata ukweli wa mazingira kwa mtuhumiwa kuachiliwa mahakamani huku akitoa wito kwa wananchi.
Kwa upande wake wakili mwandamizi mfawidhi wa serikali mkoa wa simiyu YAMIKO MLEKANO amezitaka mahakama kuangalia suala la utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa kama hao na kwamba ni vema mahakama zikawahusisha waendesha mashitaka wakati wa utoaji dhamana.
Mkuu wa hifadhi ya taifa ya serengeti,WILLIAM MWAKILEMA amesema hifadhi yake itaendelea kushikiliana na jeshi la polisi na kwamba wachache wanaopindisha sheria waache na watende haki kwa mjibu wa sheria.
Hata hivyo jangili huyo akihojiwa na waandishi wa habari amekiri kuwa amekuwa akifanya vitendo hiyo vya kuuwa tembo na kuuza meno yake na kwamba kwa sasa ameacha na akaiasa jamii kuachana na biashara hiyo.
Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakama ya wilaya ya magu ,juni 22 ili kujulishwa hukumu iliyotolewa dhidi yake.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment