Wito huo aliutoa jana katika sherehe
ya ukomo wa urushaji matangazo ya televisheni kwa mfumo wa analojia jijini Dar
es Salaam na kuwahusisha wadau mbalimbali.
Dk. Bilal alisema taasisi
zinazohusika zinapaswa kusimamia kwa ukamilifu maudhui yanayowafikia wananchi
ili yatumike kwa maendeleo na kuhakikisha kuwa channel za televisheni hazitoi
mafundisho yasiyofaa kwa vijana na kuathiri Taifa la
kesho.
“Tuna changamoto kubwa ya kutengeneza maudhui ya ndani ili tutangaze utamaduni wetu ndani na nje ya nchi kutokana na mfumo wa sasa wa digitali kujaa maudhui mengi kutoka nje,” alisema.
Aidha,alizishauri taasisi zinazohusika zikishirikiana na wadau wote kutafuta mbinu bora na kutumia fursa ya mfumo wa digitali kutengeneza maudhui yatakayotangaza nchi, utamaduni, kukuza utalii nchini na kuimarisha amani, utulivu na uzalendo.
Aliipongeza Wizara ya Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa
usimamizi na maelekezo sahihi waliyoyatoa wakati wote wa kipindi cha mabadiliko
hayo na kuvishukuru vituo vyote vya televisheni ambavyo vilitoa ushirikiano
mzuri na kuwezesha mabadiliko hayo kwa wakati.
0 comments:
Post a Comment