Kamati ya nidhamu ya FIFA ilifanya kikao chake
nchini Canada na kufikia uamuzi huo baada ya kutizama video inayomuonesha Njoku
akimpiga kumbo mchezaji wa Australia Sam Kerr katika mechi ya makundi ya kombe
la dunia la wanawake .
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alikuwa
mchezaji wa akiba na aliingia uwanjani katika dakika ya 52 ya mechi hiyo ya
kombe la dunia.
Japo tukio hilo halikuonekana na muamuzi wa mechi
hiyo, kamati hiyo ya nidhamu ilikaa kandokando ya kombe la dunia na kufikia
uamuzi huo.
Mchezaji huyo amepigwa faini ya dola elfu tatu na
mia mbili $3,200.
The Super Falcons ya Nigeria iliambulia kichapo cha
mabao 2-0 katika mechi hiyo.
Njoku sasa hataruhusiwa kushiriki mechi dhidi ya
Marekani.
Haijulikani kwanini hatua sawa na hiyo
haikuchukuliwa dhidi ya mshambulizi wa Ufaransa Camille Abily aliyempiga kumbo
mlinzi wa England Laura Bassett.
0 comments:
Post a Comment