Guinea itaviweka vijiji vinne chini ya karantini kwa siku 21,ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na masalia ya ugonjwa wa Ebola, baada ya wagonjwa wapya kugundulika kwenye maeneo hayo.
Kwa mujibu wa waraka uliotolewa na Wizara ya Afya ya nchi hiyo, vijiji vitakavyohusika na karantini hiyo ni Sikhourou Koloteya,Kusini-Mashariki mwa Mji mkuu wa Guinea,Conakry pamoja na vijiji vya Tanéné na Bamba .
Kijiji cha Tamarasy kwenye Mkoa wa Boké wenye machimbo ya madini pia kitachukuliwa hatua za kudhibiti ugonjwa wa Ebola.
Maafisa wa Afya pia watapita nyumba moja hadi nyingine kukagua wagonjwa wakati wa kipindi hicho cha karantini.
Ugonjwa wa Ebola ulisababisha vifo vya watu Elfu-11 katika mataifa ya Sierra Leone, Liberia na Guinea mwaka jana na Liberia ndiyo ilikuwa ya kwanza kuondokana na ugonjwa huo, lakini Sierra Leone na Guinea zimekuwa zikihangaika kuutokomeza ugonjwa huo.
Home
Afya
Guinea itaviweka vijiji vinne chini ya karantini kwa siku 21,ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment