Shirika
la Kutetea Haki za Binadamu la Syria,lenye
makao yake nchini Uingereza limesema,watu kadhaa wamekufa na wengine
wamejeruhiwa katika mapigano makali.
Maafiaa
wa Hospital i wanasema watu 12 wamekufa na wengine zaidi ya 70 wamejeruhiwa
hadi sasa,na kwamba mapambano yameendelea hadi leo asubuhi katika Mji huo wa
Kobane,uliopo mpakani mwa Syria na Uturuki.
Mapema
wiki hii vikosi vya Wakurdi vilisema,
vimeuteka Mji muhimu wa AIN ISSA,uliopo
Kilomita 50 kutoka makao makuu ya wapiganaji wa Islamic
State wa
Raqqa,ikiwa ni siku kadhaa baada ya kuutwaa Mji mwingine wa
Tal Abyad na kuwakatia mawasiliano wapiganaji wa Islamic State.
0 comments:
Post a Comment