MWENYEKITI wa Chama cha Mpira wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Musa
Ntimizi amemwaga vifaa vya michezo katika wilaya ya Uyui vyenye thamni
ya Sh milioni 40.
Vifaa alivyotoa kwenye timu za mpira wa miguu wilayani humo ni jezi seti 50 na mipira 200 vyote vikiwa na thamani hiyo.
Ntimizi ambaye ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora (Uyui), alitoa
vifaa hivyo kama mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya hiyo,
ikiwa ni kutimiza ahadi aliyoitoa ya kukuza vipaji wilayani kwake.
Akizungumza kwenye ziara yake wilayani Uyui, Ntimizi alisema
ataendelea kutoa vifaa vya michezo kwa timu za wilaya hiyo, kwani kuna
vipaji lukuki vinavyopaswa kuendelezwa.
“Mimi licha ya kuwa mwenyekiti wa chama cha soka wilayani kwangu,
bado ni mdau mkubwa wa soka hivyo naguswa mno kuona vijana wanakosa
fursa ya michezo ni lazima nisaidie eneo hili,” alisema Ntimizi.
Akielezea zaidi wakati akizungumza kwenye maeneo aliyopita kwenye
ziara hiyo aliwataka vijana kujitoa kushiriki michezo hasa mpira wa
miguu.
Alisema michezo ni ajira, afya, furaha na hukutanisha wadau kwa
pamoja kama ndugu hivyo yeye atakuwa pamoja nao. Kwa upande wao,
wawakilishi wa timu kwa nyakati tofauti walishukuru hekima za mwenyekiti
wa chama soka wilaya kwa hatua hiyo.
Walisema tangu historia ya wilaya hiyo kuanzishwa hawakuwahi kupatiwa msaada wa vifaa vyenye thamani kubwa kama hiyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment