BENKI ya Convenant jana ilikabidhi tiketi, mabegi ya kusafiria na
suti za michezo vyenye thamani ya Sh milioni 40 kwa Chama cha Netiboli
Tanzania (Chaneta) kwa ajili ya gharama ya usafiri kwenda Botswana
katika mashindano ya Afrika.
Timu hiyo yenye wachezaji 17 na viongozi watatu, inaondoka nchini leo
kwenda kuchuana katika mashindano hayo yatakayoanza kutimua vumbi
kuanzia Jumamosi Gaborone, Botswana.
Akizungumza wakati wa kukabidhi tiketi hizo jijini Dar es Salaam
jana, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Sabetha Mwambenja alisema kuwa,
benki yake ni ya wanawake, hivyo imeamua kuwawezesha ikiamini kuwa
michezo ni sehemu ya ajira.
Pia imefanya hivyo kwa kuwa timu hiyo ya Taifa Queens inaundwa na
wanawake ni jambo zuri kuokoa jahazi ili kuiwezesha kwenda Botswana
kushiriki mashindano hayo.
Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Annie Kibira
alisema kuwa kambi yao waliyopiga JKT Ruvu ilihitaji kiasi cha Sh
milioni 9, lakini Wizara ya Kazi, Utamaduni, Vijana na Michezo waliwapa
Sh milioni 3 tu.
Naye Allen Alex aliyewakilisha wizara inayohusika na michezo
aliishukuru benki hiyo kwa kubeba msalaba wa serikali wa kuvisaidia
vyama.
Alisema ni jukumu la serikali kuzihudumia timu za taifa, hivyo
anachukua fursa hiyo kuipongeza benki hiyo kwa kubeba jukumu hilo.
Kibira aliwataja wachezaji wanaondoka leo kuwa ni Sophia Komba, Lilian
Sylidian, Veronica Kubilu, Nasra Selemani, Chuki George, Joyce Boniface,
Jawa Idd, Faraja Malaki, Restuta Boniface, Irine Elius na Elizabeth
Fussy.
Wachezaji wengine ni Betina Kizinja, Ndigwako William, Sahriufa
Mustafa, Siwa Juma na Niza Nyange wakati viongozi ni Afsa Abrahim
(kocha), Hilda Mwakatobe (meneja) na Kibira (mkuu wa msafara).
Awali mashindano hayo yalipangwa kufanyika Namibia lakini yamepelekwa Botswana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment