Kifua Kikuu sugu, MDR-TB ugonjwa ambao unaendelea kuwa mwiba
kwa watu 480,000 duniani kote, Tanzania ikiwa ni miongoni mwao. Shirika la afya
duniani, WHO linasema kuwa MDR-TB ni ile ambayo ni sugu kiasi kwamba inagoma
kutibika kwa dawa aina za isoniazid na rifampicin, ambazo yaelezwa ni tiba
thabiti zaidi dhidi ya Kifua Kikuu. Sababu kuu za usugu ni matumizi mabaya ya
dawa hizo wakati wa matibabu, mathalani wagonjwa kuruka siku za kupatiwa tiba
au ubora duni wa dawa zenyewe. Wagonjwa wanahaha, siyo tu kwenye kusaka tiba
bali pia yale yatokanayo na tiba, mfano lishe kwani yasemekana tiba bora ni ile
iendayo sanjari na lishe bora.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment