Awali majaji wengine walitaka
sehemu ya kesi hiyo isikilizwe mji wa Bunia, kitovu cha mgogoro wa miaka mingi
kati ya makabila ya Lendu na Hema katika jimbo tajiri la mafuta la Ituri
kuwezesha waathirika kufuatilia kwa urahisi mwenendo wa kesi hiyo.
NTAGANDA anakabiliwa na mashtaka
18 ya uhalifu wa kivita na dhidi ya binadamu kwa mchango wake katika mgogoro
huo lakini mwenyewe amekanusha madai hayo.
Mahakama hiyo ambayo kwa sehemu
kubwa imeshutumiwa barani Afrika kwa kuwa taasisi inayotawaliwa na ukoloni
mamboleo wa nchi za Ulaya mara nyingi imetakiwa kusogeza kazi zake karibu na
waathirika wa vitendo vya uhalifu wa kivita na binadamu.
0 comments:
Post a Comment