Asilimia 73 ya maambukizi ya
Virusi Vya UKIMWI yanayowakumba baadhi ya vijana Barani Afrika huwapata
wasichana huku asilimia 15 ya vijana
wote ndiyo wanaotambua hadhi yao na
hivyo kusababisha tatizo hilo kuendelea
kuwa kubwa.
Hayo yamesemwa na Mke wa Rais,Mama SALMA KIKWETE alipokuwa
akizungumza kwenye mkutano wa 15 wa
Umoja wa wake wa Marais wa Afrika wa Kupambana na UKIMWI uliofanyika Sandton,
Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Mama KIKWETE ambaye ni Mwenyekiti
wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
amesema tatizo la Virusi vya UKIMWI na UKIMWI bado ni kubwa miongoni mwa
vijana wa kike na kama wataendelea kuambukizwa kwa kiwango hicho kutakuwa na
muda mrefu wa kupambana na maambukizi kwa wenzao.
Akiwakaribisha wake hao wa
Marais, Mke wa Rais wa Afrika Kusini
Mama THOBEKA MADIBA ZUMA amesema muda umefika kwa wao kuonesha majukumu yao katika Bara la Afrika kwa kuungana na viongozi
wa jamii zao ili kuondoa unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake zikiwemo mila
kandamizi, kusimamia ili wanawake wapate haki za uchumi, afya ya uzazi na
kulinda haki za wazee, walemavu na
watoto.
0 comments:
Post a Comment