Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, MAHAMOUD MGIMWA amesema hayo
alipokuwa akijibu swali la mbunge wa
Viti Maalum, PAULINE GEKUL aliyetaka
kujua ni lini kanuni za maliasili za mwaka 2011 zinazotumika kulipa fidia kwa
wananchi pale ambapo mazao yao yataharibiwa na wanyapori zitarekebishwa
kutokana na upungufu uliyojitokeza.
Amesema zoezi la kurejea kanuni
linaendelea kutokana na mchakto wake kuhusisha hatua mbalimbali ikiwemo
ushirikishwaji wa wadau mbalimbali.
Bunge limeelezwa kuwa vikundi vya
vijana 31 vimenufaika na huduma mbalimbali ikiwemo mikopo ya Shilingi Milioni 16.402,vifaa na mafunzo
mbalimbali ya ujasiriamali.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, ADAM MALIMA ametoa kauli hiyo
alipokuwa akijibu swali la mbunge wa
Viti maalum, LETICI NYERERE aliyeuliza
Serikali imetoa huduma gani kwa vijana wa wilaya ya Kwimba ili kuwezesha
kujiajiri wenyewe na vikundi gani vimenufaika na mpango huo.
Amesema kutoa huduma ya mikopo
yenye masharti nafuu kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana pamoja na kuta nyenzo
za kufanyia kazi ambapo vikundi vya vijana kutoka vijiji vitatu vilipatiwa
mashine nne za kufyatua matofali kutoka Shirika la Nyumba la Taifa.
0 comments:
Post a Comment