Naibu Waziri wa Mambo ya Nje,MAHADH JUMA MAALIM, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara ametoa kauli hiyo
alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa
Mkanyagaeni,MOHAMED MNYAA aliyeuliza
kwa nini Wizara ya Viwanda na Biashara isitoe elimu kwa wakulima namna ya
kuhifadhi matunda hapa nchni kufikia
muda angalau wa miezi mine bila ya kuharibika.
Amesema Serikali imekamilisha
jengo la kuhifadhi mboga na matunda na kuweka kontena la baridi kwa gharama ya
Shilingi zaidi ya Milioni 400
litakalohudumia vikundi 85 vya wakulima wa wilaya ya Lushoto na Korogwe.
Bunge limeelezwa Shirika la Umeme Nchni -TANESCO-
limekamilisha kuandaa hadidu za rejea kwa ajili ya kutangaza zabuni ili kumpata
mshauri mwelekezi atakayefanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa mitambo ya kufua
umeme wa makaa ya Mawe ya Ngaka itakayojengwa katika kijiji cha Ntunduwaro
Wilayani Mbinga.
0 comments:
Post a Comment