Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,
Luteini-Kanali mstaafu ISSA MACHIBYA amesema waomba hifadhi wengi ambao idadi
yao haijajulikana hawajasajiliwa na kwamba waliondoka katika maeneo ya mapokezi
hasa katika kijiji cha kagunga na kuchanganyikia na wananchi katika maeneo
mbalimbali ya vijiji hali iliyochangia kuenea kwa ugonjwa wa Kipindupindu.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Kigoma
ameeleza hayo katika kikao cha kamati ya afya ya mkoa amesema serikali itahakikisha wakimbizi hao
takriban Elfu-30 ambao wametorokea
katika maeneo mbalimbali nchini wanatafutwa na kuchukuliwa hatua za sheria.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Kigoma, Dakta LENARD SUBI
ameeleza kuwa wananchi katika vijiji vilivyokumbwa na ugonjwa wa Kipindupindu
kwa msaada wa Shirika la Afya Duniani
watapatiwa chanjo ili kuzuia ugonjwa huo kuenea zaidi.
0 comments:
Post a Comment