Idadi ya wabunge wote ni 356 na nusu yake ni 178 wanaotakiwa kupitisha jambo lolote lenye uamuzi ikiwamo miswada.
Tangu asubuhi jana, kulionekana kuwa na idadi
ndogo ya wabunge huku baadhi yao wakiingia na kutoka kila walipomaliza
kusaini mahudhurio.
Mara baada ya kupitishwa kwa muswada huo ambao
uliwasilishwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, idadi ya
wabunge ilipungua zaidi na kubaki wabunge 29 huku Muswada mwingine wa
Sheria ya Masoko ya Bidhaa wa 2015 ulipokuwa ukiwasilishwa na Naibu
Waziri wa Fedha, Adam Malima.
Wakati hali ikiwa hivyo ndani ya Ukumbi wa Bunge,
kulikuwa na idadi ndogo ya wabunge walioonekana nje ya ukumbi
wakizungumza kwa vikundi na wengine wakiwa ‘bize’ na simu zao za
mikononi.
Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Habib Mnyaa alilalamikia kitendo hicho akisema ni uvunjaji wa kanuni na Katiba ya nchi.
Mnyaa alisema kuwa wabunge wa Tanzania wengi ni
wapole na wasiopenda makuu kwani kama ingetokea mtu yeyote akasimama na
kuamua kushtaki, lazima angeshinda na kupata umaarufu mkubwa.
“Hapa tunachokifanya siyo jambo jema hata kidogo,
unajua mambo mengi tunayopitisha hapa yanakuwa sheria. Si sahihi na
tunaanza kuvunja sheria sisi wenyewe humu ndani,” alisema Mnyaa.
Alisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ibara ya 94 (1) ambayo inaeleza kuwa upitishwaji wa jambo lolote
linalohusu uamuzi wa wabunge ni lazima akidi iwe ni nusu ya wabunge wote
kama ilivyo Kanuni ya 77 ya Bunge.
“Kila tukisema sisi tunapingwa na kuambiwa kaa
chini, tena sisi wapinzani ndiyo shida kweli na hasa hawa wanaokalia
viti (anawataja) wanatubana sana ni afadhali na Ndugai (Job, Naibu
Spika),” alisema.
Mbunge huyo alibainisha kuwa wakati wowote kama
ataibuka mtu wa kutaka kuliburuza Bunge mahakamani, atashinda kesi hiyo
mchana kweupe na sheria nyingi zitapaswa kufutwa.
0 comments:
Post a Comment