Rasimu iliyopitishwa na Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma, ni
kielelezo cha wazi cha ukweli huu kwamba ujinga ni mtaji mkubwa wa
kisiasa unaotumiwa na chama tawala kwa wananchi wasiojitambua.
Hawa ni wananchi wanaoshabikia kibubusa kila kitu
kinachopendekezwa na uongozi wa CCM, hata kama ni kwa masilahi binafsi
ya viongozi wachache.
Wataalamu wa elimu wanasema kwamba ‘maarifa ni
nguvu’ Mtu ukiwa na elimu na maarifa ya kujitambua na kutambua haki zako
na nini inaendelea katika maisha yako, mazingira na nchi yako basi wewe
umekombolewa.
Hata hivyo, kuendelea kuishi katika lindi la ujinga na giza la kutojitambua, ni mtaji wa kudanganganywa na kutawaliwa.
Bunge la Katiba mpya liliendeshwa kwa msingi ya
udanganyifu, ubabe na kuukwepa ukweli uliopendekezwa na wananchi katika
Tume ya Warioba. Daima tunasema kwamba uongo hauwezi kuzaa ukweli hata
siku moja.
Ona pia suala la watangazania wa CCM, wote
wanaongea lugha nzuri na kuonyesha kutetea masilahi ya wananchi, lakini
walikuwa wapi na wamefanya nini katika kipindi chote hicho?
Wananchi waliojitambua wanauliza, kwa jinsi nchi
ilipofikia chini ya chama tawala, kuna haja gani ya kuendelea kuichagua
tena CCM inayoonyesha wazi kushindwa kuongoza nchi?
Watanzania wameahidiwa usawa wa 50/50 na katiba
mpya. Hili linawezekana katika nchi kama ya Tanzania, wakati Ulaya na
Marekani kwenyewe bado wanawake wanalalamika? Kuipitisha katiba hii ni
sawa na “kuchukua kisu na kijichinja sisi wenyewe, au kuchukua bunduki
na kujipiga risasi mguuni.
Tunahitaji katiba itakayoleta mabadliko katika
nchi yetu na katiba hii pendekezwa, haina uwezo wa kubadilisha lolote.
Hili ni suala la mfumo. Kila atakayekuja kuwa Rais kutoka CCM lazima
alinde na kuendeleza mfumo huu wa unaowalinda wachache.
Katiba ya CCM
Rasimu ya CCM iliyopitishwa Bunge la Katiba kwa
ujasiri mkubwa imeondoa uwazi na uwajibikaji kwa viongozi wake. Katiba
pendekezwa inataka kuendeleza usiri na viongozi kujifanyia mambo
kiholela holela kama wanavyotaka wao kwa manufaa yao, familia zao na
marafiki zao.
Katiba hii ikipita wananchi hamtakuwa na uwezo wa
kuwawajibisha viongozi wenu kama yalivyopendekeza maoni ya Rasimu ya
Mzee Warioba.
0 comments:
Post a Comment